Huduma ya Maji

UBORA NA USAMBAZAJI WA HUDUMA YA MAJI
Maji yanayozalishwa na DAWASCO yanakidhi viwango vya kimataifa kama ilivyoanishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia dawa zinazotumika kusafisha na kutibu maji zimethibitishwa kwa matumizi ya Binadamu. Uagizaji wa dawa zote za kusafisha na kutibu maji hupata kibali cha Mkemia Mkuu wa Serikali. Usambazaji wa maji hufanyika kwa mgao katika maeneo yote ya jiji baada ya Maji kuingia katika matanki ya kuhifadhi maji maeneo ya Kimara kwa Mtambo wa Ruvu Juu na Chuo Kikuu cha Ardhi kwa Mtambo wa Ruvu Chini. Huduma ya mgawo wa Maji imepangwa kwa ratiba maalumu kwa maeneo yote ya jiji kupata huduma ya Maji walau mara mbili kwa wiki kwa wastani wa saa 8 hadi saa 12 kwa siku. Mgawo huu hutegemea pia hali ya kujaa kwa matanki ya kuhifadhi Maji na kipindi cha majira ya mwaka.

CHANGAMOTO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA
1. Mahitaji ya Maji yanazidi uwezo wa uzalishaji wa mitambo iliyopo.
2. Mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa vyanzo vya Maji. 3. Ongezeko la gharama za Uzalishaji na Uendeshaji.
4. Wateja kutolipia ankara za matumizi ya Maji.
5. Ongezeko la idadi ya watu na Makazi yasiyo kwenye mpangilio.
6. Upotevu mkubwa wa Maji.
7. Wizi wa Maji.
8. Wizi wa Miundombinu ya Majisafi na Majitaka kutokana na biashara ya vyuma chakavu.
9. Uchakavu wa mitambo na mifumo ya maji safi na majitaka.
Karibu katika Tovuti mpya ya DAWASCO >>> Lipa ankara yako sasa kupitia Tigopesa, Mpesa, EasyPesa,Air
ARROW ARROW ARROW ARROW ARROW
Innovations > Projects > Services > Brochures > Programs >
           ARROW MGAO WA MAJI            ARROW DOKEZO NA USHAURI            ARROW ENEO LA HUDUMA            ARROW MALALAMIKO
           ARROW DIRA ZA MAJI            ARROW HUDUMA YA MAJI            ARROW MATANGAZO            ARROW MASWALI
           ARROW USOMAJI DIRA            ARROW HUDUMA YA MAJITAKA            ARROW KALENDA            ARROW TOVUTI
           ARROW MAOMBI MAPYA            ARROW MKATABA WA HUDUMA            ARROW VIPEPERUSHI            ARROW MAWASILIANO
For enquiries , complaints and emergencies please call 0800110064 (toll free) DAWASCO Call Center unit.